Danielle van de Donk alifungia Arsenal mabao mechi 20 msimu uliopita |
Ni mabingwa watetezi wa Kombe la FA
Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa Arsenal waliwalaza wapinzani wao
Tottenham 10-0 na kufika robo fainali Jumapili.
Danielle van de Donk alifungia wenyeji hao mabao matatu, naye
mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth Mead akafunga bao pia mechi yake ya
kwanza kuchezea Arsenal.
Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia
walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0.
Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda
kwenye mechi hizo za raundi ya tano.
0 comments:
Post a Comment