BAADHI YA CHUPA ZA COCACOLA ZAGUNDULIKA KUWA NA KINYESI

 Polisi wameanzisha uchunguzi wa kile kilichoonekana kuwa ni kinyesi cha binadamnu, kupatikana kwenye chupa za soda iliyowasilishwa kwa kiwanda cha Coca Cola huko Ireland kaskazini.
Shughuli za usiku katika kiwanda cha Lisburn zilivurugwa wiki iliyopita baada ya mashine kukwama.
Kampuni hiyo ilisema kuwa kisa hicho hakikuathiri vinywaji vyovyote ambavyo kwa sasa viko sokoni.
Msemaji wa Coca-Cola amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifahamu kisa hicho cha mikebe mitupu katika kiwanda cha Knockmore.
"Tatizo hilo lilitambuliwa mara moja na bidhaa zote zilizoathirika kuzuiwa na haziwezi kuuzwa. Hiki ni kisa kilicho kando na hakiathiri biddaa zozote zilizo sokoni." Alisema msemaji wa Coca Coa


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment