Agizo la ubomoaji wa nyumba ambazo zimejengwa ndani ya mita 30 kutoka kwenye hifadhi ya reli limeendelea kutekelezwa ambapo leo wakazi wa Kurasini wamekutwa na balaa hilo. Ni siku kadhaa tangu zoezi hilo lianze ambapo katika eneo la Buguruni zaidi ya nyumba 250 zilibomolewa, bomoa bomoa hiyo inayoendelea ni katika kuboresha njia za reli na usafiri wake katika jiji la Dar es saalaam
|
Katapila likibomoa majengo ya Baa ya Pentagon katika oparesheni ya bomoa bomoa nyumba zote zilizojengwa katika hifadhi ya Reli ya Kati eneo la Mivinjeni, Kurasini Dar es Salaam.
|
|
Wataalamu wakipima mita 20 kutka kwenye reli ili nyumba na mabanda yaliyo ndani ya hifadhi ya reli zibomlewe kupisha ujenzi wa reli ya kisasa. |
|
Makontena ya biashara yakiwa yamefumuliwa na
katapila |
|
Wafanya biashara ndogondogo na baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiangalia zoezi la ubomoaji likiendelea |
|
Katapila likiendelea na
kazi ya bomoa bomoa
|
|
Baa ya Pentagoni ikiwa
imebomolewa
|
|
Askari wakilinda doria wakati wa ubomoaji, kuhakikisha uwepo wa usalama katika zoezi hilo |
0 comments:
Post a Comment