Mpango wa
usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano
umezinduliwa rasmi tarehe 21 machi 2017 katika viwanja vya Kalangalala Geita
ambapo mikoa miwili yaani Geita Mwenyeji na Mkoa wa Shinyanga kwa pamoja
ulizindua mpango huo katika viwanja hivyo.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi hapo jana Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison
Mwakyembe amesema kwa sasa Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha kila mtoto
atakayezaliwa na wale wenye umri chini ya miaka mitano watapatiwa vyeti vya
kuzaliwa bure kama ilivyo elimu na chanjo na hivyo kusaidia upatikanaji wa
takwimu sahii kwa ajili ya mipango mbalimbali ya maendeleo ya Nchi kwa mfano
Serikali itajua kwa usahihi watoto wanaotakiwa kuanza darasa la kwanza pamoja
na huduma za afya,"hivyo ndugu zangu wananchi wa Geita na Shinyanga jambo
hili ni muhimu sana kwa ajili ya watoto wenu wasije kupata usumbufu hapo
baadaye watakapo anza darasa la kwanza kwani wataulizwa vyeti vya kuzaliwa pia
bima ya afya na baadaye elimu ya juu na ajira ni lazima vyeti vya
kuzaliwa."
Mpango huu
unaratibiwa na RITA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
kimataifa na kutekelezwa kupitia Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa ukiwa na
lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi kwanai usajili unafanyika
katika vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya Mama na Mtoto pamoja na ofisi za
watendaji wa kata nkatika halmashauri zote za Mkoa wa Geita na Shinyanga.
Matarajio yetu ni kusajili watoto wenye umri huo wapatao laki sita (600,000) kwa mikoa yote miwili kwani tunategemea wazazi wengi watajitokeza kutokana na wepesi wa upatikanaji wa huduma hii na hakutakuwa na malipo yoyote CHETI NI BURE, na pia urahisi wa upatikanaji wa taarifa mara baada ya mtoto kusajiliwa taarifa zake zitatumwa kwa njia ya simu maalum ya mkononi hadi kwenye kanzi data ya RITA makao makuu na mzazi atapatiwa cheti hicho papo hapo.
Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
Mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa Mkoa wa Geita
na Shinyanga. Wengine katika picha mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga (Kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.
Zainabu Telack.
0 comments:
Post a Comment