Ronnie Moran |
Nahodha na mkufunzi wa
zamani wa Liverpool Ronnie Moran amefariki dunia akiwa na umri wa miaka
83.
Moran alichezea klabu hiyo mechi 379 kati ya
1952 na 1966 pia likuwa mfanyakazi aliyehudumia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi
alipostaafu 1999.
Alijiunga
na benchi la wakufunzi Liverpool mwaka 1966 na mara mbili alihudumu kama meneja
wa muda baada ya Kenny Dalglish kujiuzulu 1991 na Graeme Souness alipofanyiwa
upasuaji wa moyo 1992.
Alihudumu chini ya mameneja tisa tofauti
alipokuwa benchi la kiufundi. Aliwaongoza Liverpool fainali ya Kombe la FA
wanjani Wembley mwaka 1992 akiwa meneja wa muda meneja wao Souness alipokuwa
anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
0 comments:
Post a Comment