CCM KUFANYIA MABADILIKO NDANI YA CHAMA




Miongoni mwa mambo yaliypitishwa leo kwenye mkutano huo maalum wa CCM ni mabadiliko ya katiba ya chama hiko ambapo mabadiliko yanayofanywa awamu hii, ni mara ya 16 "Hivyo ni desturi yetu kubadilika ili kukiimarisha chama zaidi" alisema katibu wa chama hiko ndugu. Abdularahman Kinana alisisitiza kwa kusema "mabadiliko ya CCM hayajaletwa na mtu au kikundi cha watu bali ni ya wanachama na hayamlengi mtu bali kuboresha chama".

Katibu mkuu CCM taifa ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza 




Katika mkutano huo mabadiliko ya katiba ambayo yameadhimiwa yanahusu mabadiliko ya katiba ya chama, kanuni za uchaguzi na kanuni za jumuiya za CCM (UWT, wazazi na UVCCM). Kwenye katiba ya chama hiko mabadiliko yanalenga kupunguza idadi ya wajumbe kwenye vikao, kupunguza idadi ya vikao na kupunguza utitiri wa vyeo.


Lakini pia mabadiliko ndani ya chama hiko yatahusika moja kwa moja na maendeleo ya kiuchumi katika serikali ambapo baadhi ya mipango inayotekelezwa ikiwa ni sera za ilani ya CCM 2015/2020. Mwenekiti wa CCM taifa Dkt. John Pombe Magufuli alisema "mkoa wa Pwani pekee kuna viwanda vikubwa 83 na viwanda vidogo zaidi ya 200, hii ni ishara nzuri kuelekea Tanzania ya viwanda" lakini pia kwa mwaka mmoja uliopita serikali ya Tanzania imefungua balozi mpya 6 katika nchi mbalimbali ili kuimarisha ushirikiano.

Mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza


Pamoja na hayo Mwenyekiti wa CCM taifa ameupa ukumbi wa mikutano wa CCM KIKWETE HALL, lakini pia viongozi wapya ambao wametajwa katika mkutano huo ni pamoja na Dk Abdallah Juma, Naibu katibu Mkuu Zanzibar, Perreira Silima, Katibu wa Oganaizesheni na Dk. Haule Katibu wa Uchumi na Fedha.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment