WALIOBOMOLEWA BUGURUNI KUILIPA RAHCO

Taharuki ilizuka hapo jana ambapo wakazi waliojenga nyumba zao ndani ya hifadhi ya reli katka eneo la Buguruni kuvunjiwa nyumba zao na kubaki bila makaz, zaidi ya nyumba 250 zmebomolewa, zoezi hilo linaendelea kupisha uboreshaji na ujjenzi wa reli mpya ya kisasa.


Nyumba hizo zaidi ya 250 zimebomolewa ukiwamo ukuta wa kiwanda cha Bakhresa uliokuwa ndani ya mita 30 kutoka ilikopita reli ya kati ambapo kiwanda hiko kimepewa siku tano kuubomoa ukuta huo. Licha ya hasara waliyoipata wakazi wa eneo hilo kwa nyumba zao kubomolewa, wakazi wa Buguruni waliobomolewa nyumba zao watalazimika kuilipa RAHCO kwa kuingia gharama za kubomoa nyumba hizo.



Agizo la kubomoa nyumba ambazo zipo ndani ya eneo la hofadhi ya reli, mita 30 kutoka ilipoengwa reli lltolewa miezi minne iliyopita kwa wakazi wote waliojenga mita 30 kutoka ilipoengwa reli kubomoa nyumba zao kwa gharama zao wenyewe.



Baadhi ya vyombo vya wakazi wa eneo la Buguruni ambavyo vimeokolewa.

Baadhi ya wakazi wakiwa katika hali ya butwaa kutokana na bomoa bomoa hiyo


Sehemu ya nyumba ya makazi ambayo iljengwa kwenye hifadhi ya reli ikiwa imebomolewa.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment