DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE KUZINDUA TAASISI YA MAENDELEO



Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuzindua taasisi ya maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) kesho katika hoteli ya Hyat Kempisk The Kilimanjaro Dar es salaam, baada ya uzinduzi huo Dkt. Jakaya Kikwete ataongoza kikao cha kwanza cha bodi ya taasisi hiyo.

Taasisi hiyo italenga kufanyia kazi katika maeneo yafuatayo, Maendeleo Endelevu ikiwemo kupiga vita umasikini, kusaidia wakulima na mazingira, eneo lingine ni afya ya mama na mtoto, kupambana na malaria na kuboresha lishe, eneo la tatu litakuwa ni elimu takayojumuisha elimu kwa vijana, kukuza vipaji, ujasiriamali na mafunzo, na eneo la mwisho ambalo taasisi hii itashuhulika nalo ni amani na utawala bora.

Taasisi hiyo imesajiliwa na itakuwa chini ya bodi ya wadhamini wa kimataifa yenye wajumbe kutoka ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Guinea Bisau na Marekani.

Wajumbe kutoka Tanzania ni aliyekuwa Katibu mkuu kiongozi, Ombeni Sefue, Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekeza Mukandara, Daktari bingwa wa upasuaji, Profesa William Mahalu, Balozi Mwanaidi Maajar, Genevive Sangundi, na mkurugenzi mtendai wa kundi la makampuni ya SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa.



Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment