DIAMOND NA ALI KIBA WAKUBALI KUREKODI NYIMBO MOJA

“tayari msanii Ali Kiba na Diamond wamekubali kurekodi nyimbo hiyo na wameahidi kufanya haraka  kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almas, Darasa na Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao” amesema Kitenge.

Kuelekea fainali za kombe la mataifa Africa kwa viana chini ya miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa na wasanii Chalres Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na wasanii maarufu wa muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond na Ali Kiba maarufu kama King Kiba pamoja na wasanii wengine.

Wimbo huo wa pamoa ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon ambapo zitapatikana nchi nne zitakazokwenda kombe la dunia la vijana nchini India.

Hilal amesema kuwa hatua hii ya kusaidi Serengeti Boys kutawajenga vijana hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Africa kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupata kambi ne ya nchi na kucheza mechi kadhaa za kirafiki kuto nchi za jirani lakini hata hivyo wanafikiria kutafuta mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwaaga.
Mjumbe wa kamati hiyo, Maulid Kitenge amesema kwamba tayari ala zawimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti.

“tayari msanii Ali Kiba na Diamond wamekubali kurekodi nyimbo hiyo na wameahidi kufanya haraka  kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almas, Darasa na Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao” amesema Kitenge.
Ali Kiba na Diamond wote wapo kwenye kamati iliyoundwa na waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganishawatanzania kwa pamoja ili kuhakikisha Serengeti Boys inafuzu fainali za Africa nchini Gabon mwaka huu.   

Katibu wa kamati hiyo Mwesigwa Selestine ambaye pia ni katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe wakiwa ni Maulid Kitenge, mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano na mrembo wa Miss Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo pia mkurugenzi wa habari katika wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na mkurugenzi wa vipndi Clouds radio na TV, Re Mutahaba.
Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys, Charles Hilal akizungumza na waandishi wa habari, wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya airtel Beatrice Singano akifuatiwa na mkurugenzi wa habari katika wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo, Hassan Abbas.


Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys, Charles Hilal akiwa na mjumbe wa kamati hiyo Maulid Kitenge wakiwasikilizisha wimbo wa hamasa kwa aili ya Serengeti Boys. 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment