WAYNE ROONEY NA HARRY KANE WAPATA MRITHI


Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney na Harry Kane wamepata mrithi atakayeziba pengo la uwepo wao kutokana na maeruhi waliyoyapata. Rooney na Kane walitarajiwa kuwa katika kikosi cha timu ya Uingereza kitakachovaana na timu ya taifa ya Ujerumani katika mechi ya kirafiki kabla ya mchuano wa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania huko Wembley tarehe 26 mwezi Machi.
 Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford anatarajiwa kuwa kwenye kikosi cha kocha wa Uingereza, Gareth Southgate kuziba pengo la wachezaji hao. Kiungo huyo ambaye ana umri wa miaka 19 hapo awali alitarajiwa kushirikishwa katika upande wa vijana mwenye umri chini ya miaka 21 watapokuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Denmark wikendi ijayo.

Rashford ambaye mechi yake ya kwanza kuichezea Uingereza alifunga goli walipopata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Australia mwezi Mei mwaka Jana na wamejizolea vikombe sita vikuu.
Manchester United ilimchezesha waliposhindwa kwa bao 1-0 dhidi ya Chelsea katika kombe la FA siku ya Jumatatu , licha ya kutolewa katika kikosi cha hapo awali kutokana na maradhi.Nahodha wa Uingereza, Rooney alikuwa nje wakati Manchester United ilipo kutana na Chelsea kutokana na jeraha alilolipata alipogongana na mwenzake walipokuwa wakifanya mazoezi.
Na mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane pia alitolewa nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu walipokuwa wakicheza na Millwall siku ya Jumapili. Klabu ya Spurs imesema jeraha hilo linafanana na lile alilolipata mwezi Septemba wakikabiliana na Sunderland

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment