FORBES YATAJA MATAJIRI 25 KUTOKA AFRIKA DEWJI ABAKI KUWA TAJIRI MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI KWENYE ORODHA HIYO

Jarida la Forbes limetoa majina ya matajiri 2033, huku barani Africa mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida hilo.
Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya dola 12.2 bilioni.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020. Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.
 Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017
1. Aliko Dangote, Nigeria-Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini-Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria-Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini-Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri-Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini-Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland-Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri-Utajiri: $3.8 bilioni
9. Isabel dos Santos, Angola-Utajiri: $3.1 bilioni
10. Issad Rebrab, Algeria-Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri-Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini-Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini-Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco-Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri-Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini-Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri-Utajiri: $1.76 bilioni
18. Folorunsho Alakija, Nigeria-Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco-Utajiri: $1.58 bilioni
20. Mohammed Dewji, Tanzania-Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini-Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri-Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri-Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri-Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini-Utajiri: $1 bilioni


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment