Ndani
ya mwaka wangu wa uongozi wangu Dar, nimekumbana na changamoto mbili. Kwanza
muda umekuwa hautoshi kuwahudumia wananchi
Changamoto ya pili, ni
namna ya mazoea ya watumishi wa serikali katika kuwahudumia wananchi. Tatizo la
kwenye Kata linamfikisha mtu Mkoani.
Tulifanya
uhakiki wa silaha, hili limesaidia kupunguza matukio ya kutumia silaha na
kuwamaliza waliokuwa wanajiita Panya Road.
Acha
wanaonichukia waendelee kunichukia, sina sababu ya kupendwa na mtu lakini niwe
na uhakika na safari yangu ya mbinguni.
Nawataka
wakazi wa Dar es Salaam wajue kuwa hatufanyi tunayofanya sababu ya chuki na
mtu, lakini kwa vile tunawatakia yaliyo mema.
Makundi
2 yaliyokuwa yanasumbua, ni wapiga dili wa bandari na wauza dawa za kulevya.
Wapigaji wa bandari walikuwa wanashrikiana na TRA.
Mzigo
ukija haulipiwi kodi na sokoni wanajipangia bei. Kundi la pili ni wauzaji wa dawa za kulevya. Walikuwa huwezi
kushindana nao kwenye kununua kitu, na sisi tusio na fedha wadada hawakututaka.
Kundi jingine dogo ni wenye maduka ya kubadilishia fedha. Tumeongea na Waziri
wa fedha, tunayahakiki, wiki ijayo mtasikia moto utawaka.
Dar
es Salaam tunataka kuanzisha mfumo wa kulipia kwa njia ya kadi. Hii itasaidia
kila mtu kula kwa jasho lake na tupate kodi
yumba
70% Dar es Salaam zimejengwa bila vibali na kuifanya serikali kukosa mapato
halafu kuna mijitu inajizungusha kwenye kiti ofisini.
Mtu
ukipewa kibali cha kujenga ukianza mara watu wa 'fire' wanakuja, kidogo OSHA
wanakuja, sasa unajiuliza kibali ulichopewa ni cha nini?
Nataka
watendaji mjipange, ukitoa kibali, toa kibali kimoja chenye kila kitu
(Manispaa, Zimamoto, OSHA) tuache huu mlolongo mrefu.
Mimi
sina tatizo na idadi ya watu wanaonichukia, ninachohitaji ni kutekeleza
majukumu yangu niliyopewa na Rais Dkt Magufuli
Nafahamu
kuna wamiliki wa nyumba wamelipwa fidia wabomoe nyumba zao lakini wao
wakapangisha kwa watu wengi, tutawashughulikia wote.
Tumepata
msaada wa ekari tatu ambazo tutajenga kituo kikubwa cha kuwasaidia waathirika
wa dawa za kulevya ili waondoke mitaani walipo sasa.
Vyombo
vya habari navishukuru sana, haijalishi mliandika vibaya au vizuri, lakini kwa
vile mliandika kuhusu dawa za kulevya, basi tupo wote.
Kuna
watu tuliwakamata wakasema hawatumii dawa za kulevya, tulipowaweka ndani siku
mbili hadi sauti ikabadilika wanataka kwenda hospitali.
Tunajua
baadhi yenu tukiwaita mnatumia Colgate na Chumvi ili tukikupima tusione dawa za
kulevya, tuna mbinu mpya ya kuwakamata msijisumbue.
Wauzaji
dawa za kulevya najua mmepungua, wengine mmekimbia mnapigiana simu kuulizana
hali imepoa?, kuanzia kesho kasi inaongezeka mara mbili
Kuna
Mtanzania amewekwa rehani Brazil, ndugu yake kaja kakopa benki ya Posta
kafungua duka la nguo. Ila thamani ya duka na mkopo haviendani.
Rais
Magufuli ni zawadi kutoka kwa Mungu, na mara nyingi zawadi kama hizi
hatuzielewi hadi muda wake utakapokwishi ndio tutakuja kumuelewa.
0 comments:
Post a Comment