Shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetoa majina ya wachezaji 26 ambao
watakuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ambacho kinatarajiwa kuingia kambini
mnamo tarehe 9 mwezi Machi mwaka huu wa 2017.
Kikosi
hiko chenye wachezaji ishirini na sita wakitokea timu za ndani na nje ya nchi
ikiwemo KRC Genk ya Ubelgiji anayochezea ,mshambuliaji Mbwana Samtta, AFC
Eskistuna ya nchini Sweden anayochezea mshambuliaji Thomas Ulimwengu na
Teneriffe ya nchini Hispan anayochezea kiungo Farid Musa.
Kwa timu za hapa
ndani, wachezaji ambao wanatoka timu ya Azam FC ni wachezaji saba ambao ni
AIshi Manula (Kipa), Shomari Kapombe (Mlinzi), Gadiel Michael (Mlinzi), Erasto
Nyoni (Mlinzi), Himid Mao (Kiungo), Salum Abubakar (Mlinzi), Frank Damoyo
(Mlinzi), timu ya Simba imetoa jumla ya wachezaji ambao ni Mohamed Hussein
(Mlinzi), Abdi Banda (Kiungo), Jonas Mkude (Kiungo), Said Ndemia (Kiungo),
Muzamil Yasin (Kiungo), na Shiza Kichuya (Kiungo), wachezaji kutoka timu ya
Yanga ni Deogratius Munishi (Goli Kipa), Hassan Kessy (Mlinzi), Vicent Andrew
(Mlinzi), Simon Msuva (Kiungo), timu ya Mtibwa Sugar ametoka Said Mohamed (goli
kipa), Salim Mbonde (Mlinzi), Kagera sugar ametoka Mbaraka Yusufu
(mshambuliaji), Ruvu shooting ametoka Abdularahman Mussa (Mshambuliaji), pamoja
na Mwadui FC ambako ametoka mchezaji Hassan Kabunda (kiungo).
Hii ndio orodha kamili
ya kikosi hiko;
GOLI
KIPA
AIshi
Manula (Azam FC)
Deogratius
Munishi (Yanga SC)
Said
Mohamed (Mtibwa Sugar)
WALINZI
Shomari
Kapombe (Azam FC)
Hassan
Kessy (Yanga SC)
Mohamed
Hussein (Simba SC)
Gadiel
Michael (Azam FC)
Vicent
Andrew (Yanga SC)
Salim
Mbonde (Mtibwa Sugar)
Abdi
Banda (Simba SC)
Erasto
Nyoni (Azam FC)
VIUNGO
WACHEZESHAJI
Himid
Mao (Azam FC)
Jonas
Mkude (Simba SC)
Salum
Abubakar (Azam FC)
Said
Ndemia (Simba SC)
Frank
Damoyo (Azam FC)
Muzamil
Yasin (Simba SC)
Simon
Msuva (Yanga SC)
Shizza
Kichuya (Simba)
Farid
Musa (Teneriffe, Hispan)
Hassan
Kabunda (Mwadui FC)
WASHAMBULIAJI
Mbwana
Samtta (KRC Genk-Ubelgiji)
Thomas
Ulimwengu (AFC Eskistuna-Sweden)
Ibrahim
Ajib (Simba SC)
Mbaraka
Yusufu (Kagera sugar)
Abdularahman
Mussa (Ruvu Shooting)
Hapa ndani msimu huu
timu za Simba SC na Azam FC zimeonekana zikitoa idadi sare za wachezaji ambapo
zimetoa jumla ya wachezaji saba kila timu, ikifuatiwa na timu ya Yanga ambayo
na yenyewe imetoa jumla ya wachezaji wanne, nayo timu ya Mtibwa Sugar ikitoa
wachezaji wawili, huku timu za Madui FC, Kagera Sugar, Ruvu Shooting zikitoa
mchezaji mmoja mmoja.
0 comments:
Post a Comment