Klabu ya Manchester City imetozwa
faini ya paundi alfu 35 kufuatia kulalama mbele ya mwamuzi wakati alipotoa
adhabu ya penalti kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.
Klabu ya Man city imepewa onyo kwa kushindwa kuwazuia wachezaji
wake kuwa na nidhamu uwanjani kiasi cha kumzonga mwamuzi kila wakati.
Hii inafuata tukio la dakika ya 50 baada ya mwamuzi Michael
Oliver kuizawadia Liverpool mkwaju wa penalti.
James Milner aliandika bao kwa mkwaju huo wa penalti huku Sergio
Aguero akisawazisha dakika ya 69.
Katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 Gael Clichy
alimchezea vibaya mshambuliaji Roberto Firmino wa liverpool na kusababisha
penalti hiyo
0 comments:
Post a Comment