NAPE AKABIDHI RASMI WIZARA KWA WAZIRI MWAKYEMBE

Aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa , Utamaduni na Michezo Nape Nnauye le amekabidhi rasmi wizara hiyo kwa waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Micheo Dkt. Harryson Mwakyembe. Nape alifutwa uwaziri kufuatia sakata la uvamizi wa kituo cha Clouds Media Group ambalo lilitokea siku za karibuni, hata hivyo ripoti ambayo iliandaliwa na kamati maalum kuchunguza tukio hilo tayari imemfikia waziri mpya wa wizara hiyo na ameahidi kuifanyia kazi.

Aliyekuwa waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye na waziri mpya wa wizara hiyo Dkt. Harysson Mwakyembe (walioketi) wakisaini makabidhiano ya wizara leo mapema asubihi.

  
Aliyekuwa waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye na waziri mpya wa wizara hiyo Dkt. Harysson Mwakyembe wakikabidhiana wizara kwa ajili ya kuanza kazi rasmi kwa waziri huyo mpya
                                 
Katika picha ya pamoja Aliyekuwa waziri wa Habari, sanaa, utamaduni na michezo, Nape Nnauye(wa nne kutoka kulia), waziri mpya wa wizara hiyo, Dkt. Haryson Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) pamoja na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment