Mahakama nchini Kenya imeizuia
serikali ya Kenya kuajiri madaktari 500 kutoka nchini Tanzania kutokana na kile
kilichodaiwa ni ushawishi kutoka kwa chama cha madaktari nchini humo.
Chama hiko kilikwenda
mahakamani kudai ya kwamba wapo madaktari 1,400 nchini humo ambao mpaka sasa
hawana ajira, lakini pia wamelalamikia ufujaji wa pesa kwa kile kinachodaiwa
kwamba madaktari hao watakaoajiriwa kutoka Tanzania watalipwa Tshs. 360,000 kwa siku.
Agizo hilo limetolewa na
mahakama ya kazi siku ya Ijumaa terehe.31
Machi, na litadumu mpaka ombi hilo litakaposikilizwa na kuchambuliwa.
“The leave is hereby granted,
to quash the decision of the government ..to hire foreign doctors to be deployed to Kenya” zimeandika nyaraka za
Mahakama (MachiMachi 31)
Ni wiki kadhaa tangu mgomo
wa madaktari nchini Kenya kuanza, ambapo walikuwa wakidai kuongezewa mishahara
na kuboreshewa mazingira ya kazi ikiwemo kuongezewa vifaa tiba. Siku za hivi
karibu serikali ya Tanzania ilikubali ombi la serikali ya Kenya la kuomba
madaktari ambapo serikali ya Tanzania imeahidi kupeleka madaktari 500.
0 comments:
Post a Comment