ZUMA AMFUKUZA KAZI WAZIRI WAKE WA FEDHA


Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Bwana Pravin Gordian amefutwa kazi na Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma baada ya kutuhumiwa kupanga njama za kutaka kuipindua serikali ya Zuma iliyopo madarakani.
Nafasi yake imechukuliwa na Malusi Gigaba kuwa waziri mpya wa fedha wa nchi hiyo, katika serikali ya Zuma mawaziri 15 wamefukuzwa kazi.

Waziri huyo aliamrishwa mara moja kurudi nchini Africa Kusini kutoka London alikokuwa katika ziara ya kikazi, japo wapo baadhii ya maafisa wa chama tawala cha nchini humo ANC wanaopinga kufutwa kazi kwa waziri huyo.   
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment