MARC WILMOTS |
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Marc Wilmots
ametangazwa kuwa kocha mpya wa Ivory Coast.
Wilmots
48, ametangazwa Jumanne hii na shirikisho la soka la nchini humo (FIF) kuwa
kocha wa timu hiyo akichukuwa nafasi ya Michel Dussuyer ambaye alijiuzulu mwezi
Februari mwaka huu baada ya timu hiyo kutolewa katika hatua ya makundi ya kombe
la mataifa ya Afrika yaliyofanyika nchini Gabon.
Marc alifanikiwa kuifikisha Ubelgiji kwenye hatua ya robo
fainali ya kombe la dunia 2014 yaliyofanyika Brazil na hatua ya nane bora ya
michuano ya Uefa Euro mwaka jana.
Kocha huyo atakuwa na kibarua cha kuhakikisha timu ya Ivory Coat
inafuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Urusi.
0 comments:
Post a Comment