Waziri wa maswala ya nchi za Kigeni nchini Marekani kushoto na mwenzake wa China Wang Yi |
Waziri wa maswala ya kigeni nchini
China Wang Yi ameitaka Marekani kuwa makini kuhusu mvutano wake na Korea
kaskazini. ''Hali sio nzuri
lakini haifai kulazimishwa kusababisha mzozo'',alisema baada ya kuwa mwenyeji
wa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson.
Bw Tillerson alizungumzia kuhusu viwango vya hatari vya mvutano
huo siku moja baada ya madai kwamba huenda Marekani ikaishambulia Korea
Kaskazini.
Korea Kaskazini inatengeza silaha ya kinyuklia ambayo inaweza
kufika Marekani. Wiki iliopita nchi hiyo ilizindua makombora ya masafa marefu
hatua inayokiuka masharti ya Umoja wa Mataifa.
Bwana Tillerson yuko nchini Beijing katika ziara yake ya mwisho
mashariki mwa bara Asia ambayo imetawaliwa na hali ya wasiwasi kuhusu Korea
kaskazini.
Nchini Korea Kusini siku ya Ijumaa, alisema kuwa huenda Marekani
ikaichukulia hatua Korea kaskazini iwapo itaitisha Korea Kusini ama vikosi vya
Marekani.
Rais Donald Trump alichapisha ujumbe wa Twitter akisema Korea
Kaskazini inafanya ''tabia mbaya''.
Lakini bwana Wang ametetea msimamo wa China akisema kuwa mataifa
yote yana jukumu la kutekeleza vikwazo vya UN dhidi ya Pyongyang lakini pia
zifanye majadiliano na kutoa utatuzi wa kidiplomasia.
''Tunatumai kwamba pande zote ikiwemo marafiki zetu wa Marekani
wataangazia hali iliopo kwa makini ili kufikia uamuzi wenye busara'', alisema
Wan
0 comments:
Post a Comment