Marekani
imepiga marufuku kwa muda vifaa vikubwa vya kielektoniki kama kompyuta za
kupakata, kamera, iPads visiingizwe katika mizigo inayobebwa na abiria ndani ya
ndege kutoka mataifa kadhaa ya Mashariki ya Kati.
Marufuku
hiyo vifaa vyote vya kielektroniki (isipokuwa simu) kwa abiria kutoka nchi nane
za kiislamu kuingia navyo nchini humo huku mashirka yatakayoathirika Royal
Jordanian EgyptAir Turkish Airlines Saudi Airlines Royal Air Maroc Qatar
Emirates Etihad Kuwait AirwaysSababu ya marufuku hiyo ya muda haikufahamika mara moja na maafisa wa Marekani
hawakutaka kusema chochote.
Taarifa
iliyotumwa katika mtandao wa Twitter na shirika la ndege la Saudi Airlines na
taarifa iliyofutwa ya shirika la Royal Jordanian ziliwafahamisha wateja wao
kuhusu marufuku hiyo ya vifaa vya kielektroniki vilivyo vikubwa kuliko simu ya
mkononi. Shirika la Royal Jordanian lilisema vifaa kama kompyta aina ya laptop,
kamera na vifaa vya kuchezea DVD na michezo ya kielektoniki vitahitaji
kuchunguzwa chini ya sheria mpya za serikali ya Marekani zinazoanza kutekelezwa
leo. Simu za mkono na vifaa vya utabibu vinavyohitajika ndani ya ndege
vitaruhusiwa.
0 comments:
Post a Comment