Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya soka ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kuwasili nchini
leo kuanzia Saa 4:00 usiku kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo
ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili,
kwanza na Botswana Machi 25 na baadaye Burundi Machi 28, mwaka huu Uwanja wa
Taifa mjini Dar es Salaam na pamoja na Samatta, mchezaji mwingine wa Tanzania
anayecheza Ulaya, Farid Mussa anatarajiwa pia kuwasili leo.
Wakati Samatta anayechezea KRC Genk ya
Ubelgiji atatua kwa ndege ya Shirika la Uturuki Saa 4:00 usiku, Farid wa DC
Tenerife anatarajiwa kutua kuanzia 9:00 Alfajiri kwa ndege ya KLM.Taifa Stars
itamkosa mchezaji mwingine wa Ulaya, Thomas Ulimwengu wa AFC Eskilstuna ya
Sweden, ambaye hayuko fiti.
Taifa Stars inaingia kambini leo kwenye Hoteli
ya Urban Rose, Dar es Salaam na kikosi hicho cha kocha Salum Mayanga aki
saidiwa na kocha wa Makipa, Patrick
Mwangata, Meneja wa timu Danny Msangi, Mtunza Vifaa Ally Ruvu wakati Daktari wa
timu atakuwa Richard Yomba na Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
Nyota wengine walioitwa Taifa Stars ni walinda
milango
Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi
(Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia
aliwataja
Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy
(Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel
Michael (Azam FC).
Walinzi wa kati ni
Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja
viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
Viungo ni
Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba
SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga SC)
na Shizza Kichuya (Simba SC),
Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan
Kabunda (Mwadui FC)
Wakati washambuliaji ni
Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Ajib
(Simba SC), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu
Shooting).
0 comments:
Post a Comment