Wanachama nane wa chama
cha CU, akiwemo mbunge wa Jimbo la Kaliua Tabora, Magdalena Sakaya leo
wamewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya madai iliyofunguliwa na bodi
ya wadhamini ya CUF
Pingamizi hilo la awali
limewasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa wadaiwa,
Mashaka Ngole na litasikilizwa Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri.
Katika pingamizi hilo,
wakili Ngole amedai kuwa maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na
Bodi ya wadhamini ya CUF kupitia Wakili Hashimu Mziray hayawezi kusikilizwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Amedai kuwa maombi hayo
yanashughulikiwa katika maombi namba 23 ya 2016 yaliyopo Mahakama Kuu
Masijala ya Dar es Salaam.
Ngole ameendelea kudai
kuwa, muombaji hana mguu wa kusimamia (mamlaka) ya kufungua kesi dhidi ya
wajibu maombi na kwamba maombi hayo hayana msingi kwa sababu yameshindwa
kubainisha jina la mwandishi wa masula ya fedha. Aidha wameomba mahakama
itupilie mbali maombi hayo kwa garama.
Kufuatia pingamizi hilo,
wakili Mziray aliiomba mahakama iwapatie muda wa kujibu pingamizi hilo kwa kuwa
walikwisha patiwa nakala ya pingamizi hilo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi
Aprili 12 mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza pingamizi hilo. Kesi ya msingi
imepangwa kutajwa Mei 8,2017.
Awali, Bodi ya wadhamini
ya CUF, kupitia wakili Mziray ilifungua kesi ya madai mahakamani hapo ikiomba
zuio la muda ili Sakaya na wenzake saba wasiweze kujihusisha na uongozi
wa chama na kufanya mikutano na waliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya
dharura.
Katika maombi hayo
iliyofunguliwa chini ya hati ya dharula, wajibu maombi ni Magdalena
Sakaya na wenzake Thomas Malima, Maftah Nachumu, Omar Masoud, Abdul Kambaya,
Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.
Katika maombi ya
bodi ya wadhamini wanaiomba mahakama itoe zuio la muda kwa kuwazuia
wajibu maombi ama mawakala wao au watu wao kujihusisha katika masuala
yoyote ya uongozi ama kufanya mikutano ya chama hicho, hadi maombi
yatakaposikilizwa.
0 comments:
Post a Comment