Mohammed Dewji |
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji
ameshinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa mwaka 2017 inayotolewa na Jukwaa
la Wakurugenzi Watendaji Afrika (Africa CEO Forum). Dewji ameshinda tuzo hiyo
kwa kuwashinda Abdulsamad Rabiu (CEO wa BUA Group), Issad Rebrab (CEO wa
Cevital), Naguib Sawiris ( CEO wa OTMT Investments), Said Salim Awadh Bakhresa (CEO
wa Bakhresa Group) na Strive Masiyiwa (CEO wa Econet). Akizungumza kuhusu
ushindi huo, Dewji ameishukuru Africa CEO Forum kwa kutambua mchango wake kwa
kumchagua kuwa mshindi tuzo hiyo lakini pia kuwashukuru Watanzania na Rais wa
Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kazi nzuri ya kudhibiti na kubana matumizi
mabaya ya pesa ya umma.
“Ninashukuru
sana Africa CEO Forum kwa heshima hii ambayo mmenipa, napenda kutoa tuzo hii
kwa nchi yangu Tanzania, bila wao nisingekuwa hapa na MeTL Group isingekuwa
katika nafasi iliyonayo sasa, nawashukuru sana kwa kuniruhusu mimi na familia
nzima ya MeTL kukua na kufika hapa, “Pia napenda kutoa heshima kwa Rais wangu John Pombe Magufuli anafanya
kazi nzuri na wote tunajua Afrika inavyokabiliwa na vitendo vya rushwa lakini
yeye ni mmoja wa watu ambao wanapambana na rushwa, kubana matumizi mabaya na
wenye mwono katika kazi yake.” alisema Dewji.
Aidha Dewji alisema kwa sasa bara la
Afrika uchumi wake unakua kwa kasi huku akitolea mfano wa ripoti yam waka 2015
ambayo ilionyesha uchumi wa Afrika unakua kwa asilima 4 kwa mwaka kulinganisha
na Ulaya inayokua kwa asilimia 1.5 hivyo kuwashauri wanachama wa Afrika CEO
Forum kutumia vyema fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzisaidia nchi za
Afrika kukua kiuchumi.
Tuzo za Africa CEO Forum zimetolewa
Geneva, nchini Switzerland ambapo wanachama wa jukwaa hilo wapo katika mkutano
wa siku mbili wakijadili mambo mbalimbali ambayo yanawahusu wao kama Watendaji
Wakuu na jinsi gani wanaweza kulisaidia bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment