MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA YAFANYIKA


Mazishi ya Sir George kahama yamefanyika jana tarehe 16 Machi katika makaburi ya Kinondoni,
Serikali imesema itaendelea kuenzi na kuheshimu mchango mkubwa katika kupigania maendeleo na ustawi wa jamii uliofanywa na marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika tukio la kumuaga mmoja wa waasisi wa Taifa na Waziri msataafu marehemu Sir Gorge Kahama aliyefariki dunia Machi 12 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waziri Nape amesema kuwa Sir George Kahama alikuwa kiongozi mahiri na aliyetekeleza majukumu yake kwa ufasaha ambapo alikuwa miongoni mwa viongozi walioanzisha harakati za Serikali za uendelezaji wa mji wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha makao makuu ya nchi.
“Marehemu Sir George Kahama tutamuenzi kwa kuendeleza yale mazuri aliyoyafanya katika kuijenga nchi yetu hasa katika ustawi wa jamii na kuimarisha uchumi wa nchi”.Alisema Waziri Nape.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdurahaman Kinana amumueleza Sir George Kahama kama kiongozi mahiri katika Chama aliyependa maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla katika weledi wa hali ya juu na alikuwa mchapakazi.

“Sir George Kahama alikuwa mtumishi na kiongozi aliyetukuka ametuachia hamasa kubwa ya kuwa viongozi bora zaidi na wenye mapenzi na Taifa letu katika kuleta maendeleo.”Alisema Ndugu Kinana.

Marehemu Sir George Kahama amekuwa Waziri na Kiongozi kabla na Baada ya Uhuru wa Tanzania Bara kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amezikwa leo Jijini Dar es Salaam na ameacha Mjane na Watoto.

Rai mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete wakiaga mwili wa Sir George Kahama

Mjane wa Sit George Kahama, Bi Janethe Kahama akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa mumewe 

Aliyekuwa rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akitoa heshima za mwisho jana alipokuwa akiuaga mwili wa marehemu Sir George Kahama

Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na Michezo Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Sir George Kahama
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Abdurahaman Kinana akitoa salamu za rambirambi za Chama wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Waziri mkuu mstaafu Salim Ahmed Salima kiaga mwili wa marehemu Sir George Kahama 

Aliyekuwa spika wa bunge Anna Makinda akiisalimu na kuipa pole familia ya Sir Kahama
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akitoa heshima za mwishowakati wa kuaga mwili wa Sir George Kahama

Aliyekuwa waziri mkuu wa awamu ya nne Edward Lowassa pamoja na mkewe mama Regina Lowassa wakiipa pole familia ya Sir George Kahama


Rais mstaafu wa awamu ya tatu Willium Mkapa akimpa pole mmoja wa watoto wa Sir Gerge Kahama


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment