Kikosi cha
jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza
thamani ya mazao wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo
linajilisha na kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.
Akizungumza
kaimu kamanda wa kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967
kikiwa na lengo la kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga
kiwanda cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza
uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha ulinzi kutokana na majukumu
waliyonayo.
Nkya alisema
kuwa kikosi cha 841kj kj mafinga kimeamua kujenga kiwanda hicho ambacho
kitakuwa kinaendeshwa kibiashara ili kukuza ajira na pato la taifa.
“Hapa
kikosini tunalima na kufuga mifugo ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa kiwango
kinachotakiwa kukidhi soko ili kuonyesha kuwa kikosi cha jeshi la kujenga taifa
841kj mafinga kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja ya kuanzishwa kwa kikosi
hicho”.alisema Nkya
Captain Nkya
alisema Sasa hivi Jeshi la kujenga taifa kikosi cha 841kj kimekuwa kikosi cha
Kisasa nachenye wasomi wengi wanaweza kusaidia kubuni vitu vingi vyenye faida
ya kulisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii.
“Tumefungua
kiwanda ni lazima sasa kuongeza uzalishaji kwa lengo la kuja kuipunguzia
serikali gharama za kukihudumia kikosi cha 841kj mafinga ukiangalia tunaeneo
kubwa na tunanguvu kazi hivyo ni lazima tulime na kufuga kwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli anataka jeshi la kujenga
taifa lirudi kujitegemea”.alisema Nkya
Kwa upande
wake mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale
alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 kwa kuwa kudumu
huko kwa kikosi hicho ni hatua kubwa sana katika ujenzi wa taifa.
Chale
alikitaka kikosi cha 841kj kurudisha uzalendo kama zamani ili kuendelea
kuzalisha chakula kwa wingi kama zamani kwa saizi kikosi hicho kin alima eneo
dogo sana kitu kinachochangia kuipa serikali wakati mgumu wa kikihudumia kikosi
hicho.
“Nimetembea
eneo kubwa sana leo lakini nimeona eneo la uzalishaji ni dogo sana hivyo
mnahitaji kuongeza uzalishaji ili kuisadia serikali kuzalisha chakula kwa wingi
nyie mna nguvu kazi hapa lakini bado sijaona mkiitumia ipasavyo”.alisema Chale
Aidha Chale
alikipongeza kikosi hicho cha 841kj mafinga kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuanza ujenzi wa kiwanda
ambacho kitaongeza ajira,uzalishaji wa bidhaa za chakula na kukuza uchumi wa
nchi kutokana na uzalishaji wake.
“Nichukue
fursa hii kuwapongeza kwa kuweza kuwa na wazo zuri kama hili la kujenga kiwanda
hapo ndio mnakuwa mnatimiza malengo ya kikosi cha 841kj mafinga kwa kukuza
uzalishaji kwa kutumia raslimali watu ambao mnao katika kiosi kuzalisha na sio
kila siku mnakuwa mnategemea msaada kutoka serikalini”alisma Chale
Chale
alikitaka kikosi kuendelea kutunza nidhamu waliyonayo na kuendelea kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli katika
jitihada zake za kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi na viwanda.
Lakini pia
kikosi hicho cha 841kj Mafinga kilizindua jarida linaloitwa uhodari ambalo
linaonesha kila kitu kinachofanywa na kilichofanywa na kikosi hichotoka
kuanzishwa kwake.
“Hongera
kikosi cha 841kj kwa Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa kwake”
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Luteni Kanali Mstaafu Pius Chale
alikipongeza kikosi cha 841kj Mafinga kwa kutimiza miaka 50 toka kuanzishwa
kwake
Jengo linalojengwa kwa ajili ya kiwanda cha
Kukoboa na kusaga nafaka za kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga.
Baadhi ya vijana waliopo kwenye mafunzo ya
awali ya kijeshi maarufu kama operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha
841kj mafinga nao walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.
0 comments:
Post a Comment