POGBA KUKOSA MECHI MBILI

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba hataweza kuchezea klabu hiyo mechi ya Ligi ya Premia Jumapili ugenini dhidi ya Middlesbrough.
Hii ni baada ya mchezaji huyo kupata jeraha kwenye misuli ya paja. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliumia kipindi cha pili cha mechi ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kati ya United na FC Rostov ya Urusi na ikamlazimu kuondoka uwanjani ambapo nafasi yake ilijazwa na Marouane Fellaini.
Manchester United walishinda 1-0 kupitia bado la Juan Mata na wakasonga hati robofainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Rostov.
Pogba mwenye umri wa miaka 24, pia anatarajiwa kukosa pia mechi za timu ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Luxembourg na Uhispania baadaye mwezi huu hata hivyo meneja wa United Jose Mourinho hakusema Pogba anatarajiwa kukaa nje muda gani.
Alipoulizwa iwapo huenda ikawa karibu wiki tatu, Mourinho alisema: "Kweli. Lakini sina uhakika, lakini kwa kweli hawezi kucheza dhidi ya Middlesbrough na hatachezea timu ya taifa."
Pogba ndiye mchezaji aliyenunuliwa ghali zaidi duniani na amefungia timu hiyo mabao saba na kusaidia ufungaji wa mengine matano katika mechi 41 alizowachezea msimu huu.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment