RAIS MAGUFULI AFUTA AGIZO LA MWAKYEMBE

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzana Dkt. John Pombe Magufuli amefuta agizo lililotolewa na Waziri Wa Katiba na Sheria, Dkt. Haryson Mwakyembe lenye sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa Kwa yeyote atakayehitaji kufunga ndoa kuanzia tarehe 1 Mei mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo mara baada ya agizo hilo kutolewa jana na waziri Mwakyembe, lengo ikiwa ni kutaka kuzuia wahamiai haramu na kuwepo kwa taarifa muhimu za watu zitakazosaidia kuweka mipango ya maendeleo endelevu.
Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo ya kufuta agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kbala ya kuondoka Ikulu ya Chamwino
 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment