MESSI KUTOCHEZA MECHI NNE NA TIMU YAKE YA TAIFA

Nyota wa Argentina Lionel Messi amepigwa marufuku mechi nne za kimataifa kwa kumtukana mwamuzi msaidizi wakati wa mechi kati ya taifa lake na Chile siku ya Alhamisi mjini Buenos Aires.
Shirikisho la soka duniani FIFA, lilitangaza uamuzi huo saa chache kabla ya Argentina kukutana na Bolivia katika mechi muhimu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.
Argentina, walionekana kumkosa sana mshambuliaji huyo wa Barcelona, na walilazwa 2-0 katika mechi hiyo iliyochezewa mji wa La Paz.
Mabao ya Bolivia yalifungwa na Juan Carlos Arce na Marcelo Martins. Argentina wanakabiliwa na hatari ya kushindwa kufuzu kwa michuano hiyo itakayoandaliwa nchini Urusi.
Timu nne za kwanza Amerika Kusini ndizo huhakikishiwa nafasi ya kucheza michuano hiyo ambapo kwa sasa, Argentina wanashikilia nafasi ya nne.
Zikiwa zimesalia mechi nne za kufuzu, Colombia walipanda juu ya Argentina na Uruguay na kutua nafasi ya pili kwa kulaza Ecuador 2-0 kupitia mabao ya James Rodriguez na Juan Cuadrado.
Argentina huenda wakatolewa nafasi ya nne iwapo Chile watafanikiwa kuwalaza Venezuela baadaye.

Uruguay watakuwa pia uwanjani dhidi ya Peru nao Brazil wanaoongoza wakutane na Paraguay.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment