Wengi tumekuwa tukitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika
kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida za nyanya chungu kiafya. Nyanya
chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin
A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuobresha afya ya mwili kwa
ujumla.
Ngogwe au nyanya chungu husaidia sana katika kuongeza nguvu za
uzazi kwa wanaume na inatibu pia wale wenye ugonjwa wa ngiri. Hizi pia ni
kinga iayoweza kumwepusha mlaji kupata maradhi ya moyo. Kwa wagonjwa wa
kisukari nyanya chungu pia ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango
cha sukari ndani ya mwili.
Mbali na sifa hiyo ya ngogwe/nyanya chungu pia husaidia kuongeza
stamina na uwezo wa kuvumilia na kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu
kati ya mume na mke wote endapo watakuwa wanatumia nyanya chungu katika
utaratibu unaotakiwa kitaalam (mchemsho) .
Mbali na hayo, ngogwe ni dawa inayofanana na antibiotic, hivyo ni
tunda zuri endapo likitumiwa mara kwa mara husaidia kuua vijidudu vya aina
mbalimbali mwilini.
Vitamin K inayopatikana ndani ya nyanya chungu inasaidia kuipa
nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika
mwili wa binadamu. Licha ya
kuwa karibu asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji mboga hii pia inajumuisha
madini ya chuma na potassium.
0 comments:
Post a Comment