CCM YATEUA MAJINA 12 YA WANACHAMA WATAKAOWANIA UBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI


Kamati Kuu Leo tarehe 29/3/2017 imefanya kikao na kupokea, kujadili na kupitisha majina ya wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki na kuteua majina 12 ya wanachama kutoa chama hiko watakaowania nafasi tisa za uwakilishi wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki.

Uteuzi huo umezingatia mageuzi yanayolenga kuimarisha misingi ya uadilifu, uwajibikaji, uchapakazi, uwakilishi unaozingatia usawa na Utaifa. Naye mwenyekiti wa chama hiko amewapongeza wanachama wote walioomba ridhaa ya ubunge wa bunge la Afrika Mashariki na kuahidi kuwatumia kama hazina.

Uteuzi huo umezingatia usawa wa wagombea kutoka Tanzania bara na visiwani, alkini pia katika upande wa jinsia.  Idadi kamili ya wagombea walioteuliwa kutoka Tanzania bara n inane, wanaume wanne na wanawake wane, kutoka Tanzania visiwani ni wagombea wane, wanawake wawili na wanaume wawili.
Orodha ya walioteuliwa na Kamati Kuu;
Wanaume Tanzania Bara
1. Dr Ngwaru Maghembe.
2. Adam Kimbisa.
3. Anamringi Macha.
4. Charles Orodha ya walioteuliwa na Kamati Kuu;
Wanawaeke kutoka Tanzania Bara
1. Zainab Kawawa.
2. Happiness Lugiko.
3. Fancy Nkuhi.
4. Happiness Ngoti Mgalula

Wanaume kutoka Zanzibar
1. Abdalla Hasnu Makame.
2. Mohamed Yussuf Nuh.
Wanawake kutoka Zanzibar
1. Maryam Ussi Yahya.
2. Rabia Abdalla Hamid.
Katibu wa itikaadi na uenezi wa CCM alisema kwamba katika mchakato huo wanachama wengi walijitokeza, huku idadi kubwa ikiwa ni wasomi kutoka vyuo vikuu
“Katika mchakato huu, wanachama 450 walijitokeza, wanawake 93 na wanaume 357, wengi wakiwa na elimu ya Chuo Kikuu
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment