Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo
amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa
Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za
kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa
mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau
Bunge.
Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia
Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe.
Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexandra Mnyeti na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya
Kudharau Bunge
RC Makonda alipokuwa akiwasili bungeni
na kupokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Bungeni, Owen Mwandumbya kuitikia
wito wa Kamati ya Bunge
|
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es
Salaam Paul Makonda akihojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga &
Madaraka kujibu tuhuma zinazomkabili.
|
0 comments:
Post a Comment