Watuhumiwa Sultan
Ibrahimu kulia na Ramadhani Hamisi wakijiandaa kushuka kutoka kizimbani Mara
baada ya kesi yao ya kuingiza magari kwa kificho na kuisababishia serikali
hasara ya zaidi ya milioni 287.8 kuahirishishwa
Na Karama Kenyunko, blogu
ya Jamii.
Wafanyabiashara watatu
akiwemo raia wa Zambia mmoja wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za
uhujumi uchumi ikiwemo kusafirisha bidhaa kwa kificho.
Washtakiwa hao ambao
wamefikishwa mbele ya Mahakimu wawili tofauti ni Sultani Ibrahimu, (36),
mwarabu Mkazi wa Usalama Temeke, Augustino Kalumba (39) raia wa Zambia na
Ramadhani Hamisi maarufu kama Ukwaju (48) anaishi Kinondoni Hananasifu.
Wanadaiwa kutenda makosa
hayo kinyume na sheria ya Umoja wa nchi za Afrika Mashariki ya kudhibiti
ushuru.
Mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Thomas Simba washtakiwa Sultan Ibrahimu na Augustino Kalumba wamesomewa
mashtaka matatu, la kula njama, kusafirisha Mali iliyofichwa na kuitia
hasara serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania zaidi ya shilingi
milioni 287.8.
Mwendesha mashtaka
Nassoro Katuga akisaidiana na Wakili Batlida Mushi amedai kuwa kati ya Decemba
1 mwaka jana na Machi 1 mwaka huu katika eneo lisilojulikana washtakiwa hao
wakiwa na wenzao ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya kusafirisha mali.
Katika shtaka la pili
imedaiwa kuwa kati ya Decemba 1 hadi 31, mwaka jana katika makao makuu ya
Bandari ya Tanzania yaliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa
waliingiza magari matatu ambayo ni Range Rover sports, Zenye naomba tofauti
tofauti.
Imedaiwa kuwa magari hayo
yalikuwa yamepakiwa pamoja na nguo za mitumba na viatu kwenye kontena namba
MSKU 9914168 kwa nia ya kuwadanganya maafisa wa ushuru.
Aidha washtakiwa hao kwa
pamoja wanadaiwa kuingiza Mali hizo wakiwa wamezificha na kuisababishia
serikali ya Tanzania kuingia hasara zaidi ya shilingi 287.8
Mbele ya Hakimu
Respicious Mwijage washtakiwa Sultan Ibrahim na Ramadhani Hamis wamesomewa
mashtaka matatu.
Imedaiwa kuwa kati ya
Decemba Mosi mwaka jana na March 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam, washtakiwa
hao walikula njama ya kutenda kosa la Kuficha Mzigo wakati wakiuingiza nchini.
Imeendelea kudaiwa
kuwa, kwa pamoja washtakiwa hao waliingiza Mzigo wa magari matatu wakiwa
wameyaficha ili kuweza kuwaficha maafisa ushuru.
Wakili Katuga amedai kuwa
kitendo hicho kimeikosesha serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania mapato
zaidi ya shilingi milioni 190.9
Hata hivyo washtakiwa hao
hawakuruhisiwa kujibu kitu chochote na wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka
dhidi yao yako chini ya sheria ya uhujumu uchumi ambayo Mahakama ya Kisutu
haina mamlaka ya kutoa dhamana.Aidha Wakili Katuga aliiarifu mahakama kuwa DPP
bado hajatoa kibali kwa mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Kesi hiyo itatajwa
mahakamani hapo Aprili 12 mwaka huu. Upelelezi bado haujakamilika.
0 comments:
Post a Comment