MIFUMO MiZURI YA KUFANYA KILIMO


Mifumo ya kilimo hutambulisha na kuonyesha mpangilio wa shamba, kuchanganyika au kufuatana kwa mazao kutokana na nafasi na muda, pamoja na matunzo na mbinu za uzalishaji wake. Mifumo hii hutofautiana kati ya mkulima na mkulima, au sehemu na sehemu. 

Baadhi ya aina za mifumo ya kilimo ni pamoja na
-Aina moja ya zao (Monoculture or Sole cropping), huu ni uzalishaji wa aina moja ya zao katika eneo kwa wakati mmoja. Mimea hapa hupandwa, hutunzwa na huvunwa kwa wakati mmoja. 



-Kilimo Mchanganyiko (Mixed farming), huu ni uzalishaji wa mazao pamoja na ufugaji katika eneo moja. Inaweza kujumuisha pia na ukuzaji wa mimea kwa ajili ya chakula cha mifugo. Hapa mkulima atafaidika pia na mbolea ya samadi kutokana na mifugo. 


-Mazao Mchanganyiko (Multiple Cropping or Polycropping), huu ni uzalishaji wa mazao zaidi ya aina moja katika eneo moja. Huu mfumo waweza kuwa kwa kuchanganya, kupishana, kufuatana au kwa mzunguko. 

Mkulima anaweza kupanda mazao ya aina zaidi ya moja katika eneo kwa wakati mmoja (Intercropping). Mazao yaweza kupandwa kwa mistari, kupishana, kuchanganywa au kufuatana. 

Mkulima pia anaweza kugawa eneo vipande na kupanda kila kipande zao la aina tofauti na baada ya kuvuna kila kipande hupandwa zao tofauti tena na hii inakwenda kwa mzunguko (Crop Rotation). Pia unaweza kulima mazao aina zaidi ya moja kwa msimu, na hapa mkulima anaamua kulima mazao aina mbili au tatu bila kubadili kwa msimu mzima (Sequential Cropping). 


-Kilimo Mseto (Agro-forestry), huu ni mfumo wa kuchanganya kwa mpangilio mazao ya kilimo na miti. Hapa waweza kutumia miti rafiki kwa kilimo na mifugo kama Mglirisidia, Mfudufudu au Mlonge, na/au miti ya matunda. 


Kuchagua mfumo wa kilimo itategemea na eneo lako pamoja na miundombinu na rasilimali zilizoko. Kitu cha msingi ni kuitumia ardhi vizuri kutokana na nafasi na muda ili kuvuna kwa kiwango cha juu na kwa malengo unayojiwekea.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment