Jeshi la polisi Mkoani Pwani linawashikilia watu 20 kwa kosa la kuhusika na uuzaji wa dawa mbalimbali za kulevya ikiwemo heroin,mirungi na bangi .
Aidha limekamata nyara za serikali ,meno ya tembo sita thamani yake mil.98.100 na vipande 56 vya ngozi ya mbalawa .
Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata magunia ya bangi 28, puli 270 ,heroin kete 700 ,lita 522 za pombe ya moshi (gongo) na mitambo saba ya kutengeneza pombe hiyo,misokoto 52 ,kete 2,853 na mirungi milaa 94 .
Akizungumzia juu ya matukio hayo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi alisema, pia wamewakamata wahamiaji haramu 153 ambapo kati ya hao saba walikutwa wakisafirishwa kwenye gari namba T.568 CZG .
Alieleza ,kuna mazao ya misitu yasiyokuwa na vibali nayo yamekamatwa ikiwa ni pamoja na mkaa magunia 71 na ambao 117 ,sukari viroba 23 vya kg hamsini na mchele viroba 12 vya kg 12 ,simu za mkononi 29 na nondo tani 10.
Pia, kamanda Mushongi, alisema mafanikio hayo yametokana na operesheni iliyofanyika ndani ya wiki mbili baada ya kutokea tukio la mauaji ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Liwale Ephraim Mfingi Mbaga (54).
0 comments:
Post a Comment