Carlos the Jackal, gaidi kutoka
Venezuela, anayedaiwa kuhusika katika mashambulio kadhaa Ufaransa miaka ya 1970
na 80, atashitakiwa tena kuhusiana na shambulio lililotekelezwa katika duka
moja. Mtuhumiwa huyo kwa
sasa anatumikia vifungo viwili vya maisha jela kwa kufanya mauaji kadha, kwa kile alichokidai kuwa ni kutetea
haki za Wapalestina na wakomunisti ambapo katika mahojiano na gazeti moja,
Ramirez anadaiwa kusema alitekeleza shambulio hilo kuishurutisha Ufaransa
kumwachilia huru mwanaharakati wa kikomunisti kutoka Japan.
Ramirez mwenye umri wa miaka 67, atafikishwa mbele ya majaji
watatu mahakamani mjini Paris Jumatatu kuhusiana na shambulio la guruneti
lililotekelezwa katika jumba moja la kibiashara mtaa wa Latin Quarter mjini
Paris Septemba 1974 ambapo watu wawili waliuawa na wengine 34 walijeruhiwa
wakati wa shambulio hilo.
Ramirez amekanusha mashtaka hayo na wakili wake, Isabelle
Coutant-Peyre, amesema kesi hiyo ni kupoteza wakati wa pesa bure.
Ramirez
alipatikana na makosa mengine ya kutekeleza mashambulio manne ya mabomu mjini
Paris na Marselle mnamo mwaka 1982 na 1983 ambapo watu kumi na moja waliuwawa
na wengine mia moja na hamsini kujeruhiwa. ,Mnamo mwaka 2011 na 2013 alpatikana
na hatia ya makosa hayo.
Ramirez alikamatwa mjini Khartoum na maafisa wa usalama wa
Ufaransa mwaka 1994, miaka 20 baada yake kutekeleza shambulio lake la kwanza..
Wakili
wa waathiriwa wa mashambulizi hay Georges Holleaux, amesema jamaa za waathiriwa
wanasubiri sana na wangefurahia kumuona akiwa kizimbani. "Waathiriwa wamesubiri
sana kumuona Ramirez akishtakiwa na kuhukumiwa. Vidonda vyao havijawahi
kupona," amesema.
0 comments:
Post a Comment