Inasemekana kuwa wezi wamevunja na
kuingia katika nyumba ya aliyekuwa nahodha wa timu ya uingereza John Terry
wakati akiwa katika likizo ya kifamilia.
John Terry ameripotiwa kuishi katika nyumba ya vyumba saba tofauti
nchini humo.
Polisi Surrey wamethibitissha kutokea kwa tukio hilo siku za
mwisho za juma lililopita kwenye nyuba ya mchezaji huyo iliyopo Oxshott. “Tunaweza
kuthibitisha kuwa wizi ulifanyika katika nyumba moja iliopo Moles Hill ,Oxshott
usiku wa terehe 25 na 26 mwezi Februari” alisema msemaji wa kituo cha polisi cha
Surrey.
Wezi hao wanadaiwa kuvunja na kuuingia katika nyumba hiyo na
kuiba vitu vyenye thamani wakati ambapo mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa
miaka 36 akiwa likizo na familia yake akiwemo mkewe Toni kulingana na ripoti za
gazeti la The Sun.
0 comments:
Post a Comment