Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameagiza nyumba 36
zibomolewe katika bonde la mto Msimbazi na maeneo mengine hatarishi, ili
kuondokana na janga la mafuriko.
Makonda amezitembelea nyumba hizo katika Kata ya Bugurni kwa
Mnyamani na Tabata, akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo ameshuhudia
maafa makubwa yakiwemo ya baadhi ya watu kupoteza mali pamoja na nyumba zao
kujaa maji na nyingine kubomoka kufuatia mvua zilizoanza kunyesha mwanzoni mwa
mwezi huu jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiavuka mto ambao umefurika maji alipokuwa katika ziara yake hiyo |
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akitizama sehemu ya nyumba ambayo imeboboka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha |
Mkuu wa mkoa akiwa na kikosi chake wakati wa ziara ya kutembelea wakazi wa bonde la mto msimbazi kushuhudia maafa yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha |
Pamoa na watu wengi kupoteza makazi, mali na wenigne maisha,
jambo ambalo limemgusa RC Makonda na kufikia uamuzi huo wa kuiomba Halmashauri
ya Ilala kuanza zoezi hilo la ubomoaji mara moja.
RC Makonda amesema kuna watu ambao tayari wamelipwa pesa kuhama
maeneo hayo lakini cha ajabu wengine hawajaondoka na wengine wamewapangisha
watu wengine kwenye maeneo hayo hatarishi, jambo ambalo serikali yake haiwezi
kulikalia macho na kuagiza kubomolewa kwa nyumba hizo.
Pia amewataka wale ambao hawajahakiki taarifa zao kuhusu kupewa
hifadhi baada ya nyumba zao kubomolewa wafanye hivyo kwa kwenda ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Ilala kwa uhakiki huo.
0 comments:
Post a Comment