Shirika la mpango wa chakula Duniani WFP limeanza kutoa kiasi
cha shilingi elfu 20 pesa taslimu za Kitanzania, sawa na dola tisa, kwa
wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania,
ambapo zaidi ya wakimbizi laki moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na
Burundi wamehifadhiwa katika kambi hiyo.
Hii ni mara ya kwanza kwa wakimbizi kupewa msaada wa chakula kwa
mfumo wa kupokea fedha tangu kuwepo kwa kambi za wakimbizi nchini Tanzania.
Eneo la kambi hiyo ya Nyarugusu imeonekana ikichangamka baada ya
wafanyabiashara hususani wa mazo ya chakula wakiwa wametia kambi katika kambi
hiyo, huku wakimbizi wakiwa hawana namna nyingine ya kupata chakula cha kila
siku zaidi ya kununua kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Hata hivyo wakimbizi wengi wameonekana wakifurahia utaratibu huo
wa kugawiwa pesa badala ya chakula kwa kile walichokidai kwamba hawakuwa
wakipata fursa ya kupata chakula tofauti na kile wanacholetewa na shirika hilo.
“tulikuwa tunapokea unga tulikuwa na malalamiko mengi, hatubadilishi chakula
tunaibiwa kwenye mizani lakini sasa hivi hakuna kuibiwa kwenye mizani ” alisema
mmoja wa wakimbizi.
Naye Said Johari mkuu wa shirika la umoja wa
mataifa la mpango wa chakula WFP ofisi ya Kasulu anasema “pale tulipokuwa
tunagawa chakula tulikuwa tunachukua siku tano mpaka saba kumaliza ugawaji
lakini kwa mgoa wa fedha ugawaji unatuchukua maximum siku tatu, kazi imekuwa
rahisi”
Brigedia jenerali Emmanuel Maganga mkuu wa
mkoa wa Kigoma amezungumzia suala la usalama, anasema “ muingiliano ni mkubwa
sana tunay matarajio ya kuanzisha vitambulisho vya wakimbizi”
0 comments:
Post a Comment