Nchini Marekani kumezuka muswada wa kutunga sharia ya kuzuia
upigaji penyeto (kujichua sehemu za siri) lengo la sheria hiyo ambayo hoja yake
imetolewa na,Jesica Farar ambaye ni mwanachama wa Democrat katika bunge la
wawakilishi wa jimbo la Texas anasema ni
kuwalinda watoto ambao hawajazaliwa kila mahali, anataka mwanamume atakayemwaga
mbegu zake za kiume nje ya uke wa mwanamke ama kutengemezwa nje ya kituo cha
matibabu kutozwa faini ya dola 100.
Iwapo mwanamume atapatikana na hatia kwa kumwaga mbegu hizo nje
itachukuliwa kama kitendo dhidi ya mtoto ambaye hajazaliwa. ''Iwapo inaonekana
kama hatua isio ya kawaida basi hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa''alisema Farrar.
Jessica Farrar aliuwasilisha muswada huo nambari 4260 wiki iliyopita
japo anajua hautaidhinishwa kuwa sheria,
amesema kuwa sio rahisi zaidi ya kuwawekea wanawake sheria kali za utoaji
mimba katika jimbo la Texas wakati mtu anapochagua kutaka kutoa mimba.
Sheria ya hivi karibuni ilikuwa ile inayowashinikiza wanawake
kuchagua kuzika ama kuchoma mabaki ya viinitete kutokana na mimba iliotoka ama
ile iliotolewa. Wakati wa kusikizwa kwa muswada huo mnamo mwezi Agosti, Seneta
wa jimbo hilo Don Huffines alisema: kwa muda mrefu sasa Texas imeruhusu viumbe
visivyo na hatia kutupwa na uchafu. Iwapo tunachukulia hatua hizi na umuhimu
mkubwa kwa sababu ya maisha ,basi, hatuwezi kupoteza hata mbegu moja.
Hoja hii inapingwa wazi wazi na baadhi ya watu, mtu mmoja
alituma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter akisema kuwa ''ni yai
lililorutubishwa pekee ambalo linahitaji kulindwa akiuliza iwapo angeweza
kutumia sheria hiyo dhidi ya wanawake walio katika hedhi.
Jimbo la Texas lina sheria kali za utoaji mimba nchini Marekani japokuwa
mahakama ya juu ilibatilisha marufuku juu ya utoaji mimba.
Sheria hiyo inamaanisha kwamba kliniki zinazotoa mimba ni chache
mno.
Kulingana na gazeti la Tribune katika jimbo hilo kulikuwa na
kiliniki 19 za utoaji mimba mnamo mwezi Juni 2016, nyingi zikifanya kazi katika
maeneo ya mijini.
0 comments:
Post a Comment