Wakazi zaidi ya 20 wa kata ya Vigwaza iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamegundulika kuwa na matatizo ya macho na kutakiwa kufanyiwa upasuaji ili kutibu ugonjwa wa mtoto wa jicho baada ya zoezi la upimaji lilifonyika kwa takribani siku mbili na taasisi isiyo ya kiserikali ya Lions Club Dar es salaam-Panorama ambapo huduma hiyo ya macho iligharimu kiasi cha Milioni ambapo huduma hiyo ya macho iligharimu kiasi cha Shilingi Milioni 30.
Mratibu wa taasisi hiyo Bwana Prash Bhatti alisema mbali na kutoa
huduma ya mcho, pia waliwahudumia wagonjwa wa kisukari, presha na kusaidia
huduma za kijamii, Bhati alisema kwamba kambi hiyo ilikuwa ya siku mbili ambapo
watu 2,000 walijitokeza kupima macho na kupata huduma ya miwanibure na zaidi ya
watu 20 walikutwa na motto wa jicho.
“Shida kubwa ni motto wa jicho ambayo kwa kitaalamu tunaiita cataract ugonjwa
huu ndio unaoongoza kwa kuharibu jicho, dawa yake ni upasuaji” alisema. Bhatti
alieleza kuwa, watu wote waliogundulika na motto wa jicho watafanyiwa upasuaji
na gharama zote zitatolewa na Lions Club.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Ndekilo akizungumza. |
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evaris Ndekilo, alitoa wito kwa
jamii kupima macho mara kwa mara ili tatizo libainike mapema na kutibiwa, pia
alisem tiba ya ugonjwa huo ni upasuaji na kuwa ulaji mzuri wa chakula na
matunda hukinga macho dhidi ya magonjwa.
“Nampngeza diwan wa kata hii Mohsin Bharwan kwa kuona umuhimu wa
kuwatumikia wananchi wake ikiwemo masuala ya kiafya” alisema Mhandisi Ndikilo
Diwani wa kata hiyo aliishukuru taasisi hiyo kwa kujitolea kutoa huduma
mbalimbali za afya na vitabu na madaftari kwa shule zilizopo Vigwaza.
0 comments:
Post a Comment