MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA MKOA WA DODOMA

Makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tnzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma kuondoa vitendo vya ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali, ambapo ukiritimba huo unaweza kusababisha ucheleshaji au kukwaisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa katika maendeo ya moa huo.

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kupokea taarifa ya kikosi kazi kilichoundwa na serikali kwa ajili ya kuratibu shuhuli mbali mbali za serikali kuhamia mjini Dodoma
Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi mkoa wa mkoa wa Dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto asili yasije yakaharibiwa na uwekezaji utakaofanyika.

Kuhusu maeneo ya wafanya biashara,  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu amewataka viongozi wa moa huo kuhakikisha wanatenga maeneo maalum kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

Awali kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kuzungumza na uongozi wa mkoa wa Dodoma, mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alimueleza Makamu wa Rais mipango na mikakati ya mkoa huo kuhusu azma ya serikali ya kuhamia Dodoma ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma za msingi ikiwemo afya, elimu, miundombinu, maji,na  umeme.

Mkuu wa mkoa huo wa Dodoma, aliongezea kwa kusema mpaka sasa kazi ya kuimarisha meneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji, makazi na mahala ambapo ofisi za serikali na balozi zitajengwa umeshakamilika.  

Ameeleza kuwa ujenzi wa miji mitano mikubwa mkoani Dodoma na ujio wa wawekezaji utaufanya mkoa huo kuwa na uhitaji mkubwa wa nishati ya umeme na wa uhakika hivyo amehimiza ujenzi wa bomba la gesi asili kutoka Dar es salaam ukafanyika kwa kasi zaidi. Pia amesema uongozi wa mkoa wa Dodoma utaendelea kushiriiana na mashirika na taasisi mbali mbali ili kuhakikisha maeneo yaliyojengwa yanaendelezwa haraka. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment