PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO

Mfuko wa Pensheni wa PPF, umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau. Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF. 

Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii. Wakati wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu aliungana na Bodi ya Wadhamini wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF walienda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya Afya 16 nchini vitakavyonufaika na msaada wa vifaa hivyo.
Mhe. Jenista Mhagama, alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.

“Hivi sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia hongereni sana PPF.”


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment