Makubaliano yaliyofikiwa kati
ya Wizara ya Elimu na kampuni ya IBM katika kusukuma Elimu Kwa njia ya dijitali
huenda yakaafikiwa baada ya kampuni ya vodacom kufanya uwekezaji katika
kusambaza miundombinu yake ya Minara Kwa kurahisisha huduma wa upatikanaji wa
Intanenti.
Kampuni hiyo ndiyo inayoongoza
katika sekta ya mawasiliano za simu za mkononi nchini kupitia sera yake ya
kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali na kuyabadilisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia.
Kampuni hiyo kwasasa inawafikia asilimia 88
ya watanzania ambao wananufaika Moja Kwa moja kwa huduma ya mtandao wa Vodacom
kutoka katika minara zaidi 2700 ya huduma ya 2G, Minara 2000 ya 3G pamoja na
Minara 278 ya 4G kwa Dar es Salaam, Kila mwezi vodacom Tanzania inatoa huduma
ya data nyingi zaidi ya Petabytes 2 kulinganisha na mitandao mingine kutoka na
uhitaji na idadi ya watumiaji wake kwa kadiri Intaneti inavyozidi kuongezeka na
kusambazwa kutokana kuwepo kwa idadi kubwa ya miundombinu ya minara yenye kutoa
huduma nchini.
Hali hii ya usambazwaji wa
Minara itasaidia kufikia malengo ya Wizara ya Elimu kuwaunganisha watanzania
pamoja na kutoa Fursa kupitia uwezeshaji wa Elimu pamoja kuwawezesha walimu na
wanafunzi kufaidika kutumia huduma za dijitali katika kujifunza na
kubadilishana mawazo.
Aidha hii ni nafasi ya
watanzania kufaidika kwenye sehemu ya Gurudumu hili la kuwezesha Elimu bure kwa
kununua hisa za Vodacom kulingana na huduma na uwekezaji katika kampuni ya
Vodacom Tanzania.
0 comments:
Post a Comment