Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea ripoti ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30
Juni, 2016.
Ripoti ya CAG imegusia,
hesabu za Serikali, misamaha ya kodi, ukusanyaji wa kodi, uandaaji na
utekelezaji wa bajeti, deni la Taifa, usimamizi wa mali na madeni ya Serikali,
usimamizi na uendeshaji wa taasisi za umma na mashirika, udhibiti mianya ya
upotevu wa fedha, TANESCO kutonunua umeme wa gharama kubwa na matumizi mabaya
ya misamaha ya kodi.
|
0 comments:
Post a Comment