Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera. Michezo hiyo itafanyika Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu.
Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon
itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana
Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo
utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Timu itaelekea Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye itapita Cameroon
kwenye kambi ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon katika michuano
itakayoanza Mei 14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili za kimataifa
dhidi ya wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.
Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.
Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na
Angola. Ina lengo la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
La ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali
ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali
za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.
Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na Makipa: Ramadhan Kabwili,
Samwel Edward na Kelvin Kayego.
Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson Kibabage, Israel Mwenda,
Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi, Mohamed Rashid,
Shaaban Ada, Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na
Cyprian Benedictor Mtesigwa.
Washambuliaji: Muhsin Malima Makame, Yohana Mkomola, Ibrahim
Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
Benchi la Ufundi:
Bakari Shime (Kocha Mkuu)
Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi)
Muharami Mohamed (Kocha wa makipa)
Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi)
Edward Evans (Mtunza Vifaa)
Shecky Mngazija (Daktari wa timu)
0 comments:
Post a Comment