Kiongozi huyo amemtaka waziri
mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria.
"Kila kitu chenye nia ya
uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka
ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe
kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe na
mabalozi ikulu.
"Kwa ni mwanasheria mzuri,
msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha
serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache."
Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba
ukurasa wa juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya
aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akitolewa bastola katika vurugu
zilizotokea jana.
"Hata kasomeni tu leo
magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja,
kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu
anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini.
Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."
0 comments:
Post a Comment