Waziri wa mambo ya ndani nchini
Tanzania Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari mmoja kuchomoa bastola
na kufyatua risasi wakati maafisa wa usalama walipokuwa wanajaribu kumzuia
aliyekuwa waziri wa habari kuhutubia wanahabari.
Bw Nchemba, kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kitendo
hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika kuadhibiwa.
Amesema amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha
zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumsaka mhusika.
"Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge,
mjumbe wa NEC wa CCM, hana rekodi ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea bastola,
sio cha kiasikari, sio cha Kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza
kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya
nini," ameandika.
"Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania,
nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha
kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari basi sheria zinazoongoza
taasisi husika zichukue mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment