Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni Susan Kaganda, amesema kuwa yeye hakutoa maelekezo ya kuzuia
mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye
pamoja na Waandishi wa Habari Jana Protea Hotel.
Akifafanua
kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema Leo asubuhi, Susan amedai
yeye kama Kamanda hana mamlaka ya kuingilia biashara binafsi (Protea Hotel), na
alikwenda pale kuhakikisha Usalama unaimarika zaidi na si vinginevyo.
“Protea
ni private Hotel sio Mali ya Serikali, ile ni Biashara huru kamanda hawezi
kuzuia, lakini nilikuta Waandishi wengi pale na alipata fursa ya kuongea nao.
”Mimi kazi yangu ni kusimamia Usalama wa Raia na Mali zao, mkutano unanihusu
ukiwa wa Hadhara” alisema RPC Susan.
Alipoulizwa
kuhusiana na kipande cha ‘Picha Jongefu’ (video) inayomuonyesha mtu
anayedhaniwa kuwa Askari akimtolea silaha Nape Nnauye, amesema hawezi
kuliongelea swala hilo kwa sasa mpaka uchunguzi utakapokamilika kwa maana
kipande hicho hakionyeshi Sura ya mtu Huyo.
“Jeshi
la Polisi tunawafundisha Askari wetu kutumia nguvu kwa namna wanavyokutana na
mazingira, sikuwepo sikuona nilielezwa na ndio maana nilikwenda nikamuuliza Mh
uko sawa akanijibu yuko salama,”
“Lakini
kama kuna Silaha imetumika kama ambavyo nimeona kwenye vyombo vya Habari
tunalifanyia Uchunguzi, sikuwepo eneo la tukio picha ile inaonyesha KISOGO,
kuwa mtulivu tunachunguza” alifafanu
Source; Times FM
0 comments:
Post a Comment