SHIRIKISHO LA MPIRA NCHINI UINGEREZA LAISHTAKI MANCHESTER UNITED

Wachezaji wa Mancheste United wakiwa wamemzunguka refa baada ya mchezaji mwenzao kupewa kadi nyekundu. 
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeishtaki klabu ya Manchester United kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea.
Refa Michael Oliver alizungukwa na wachezaji wa United baada ya kumpa kadi nyekundu Ander Herrera dakika 10 kabla ya muda wa mapumziko, katika mechi hiyo Manchester United ilipoteza mechi hiyo kwa 1-0.
Kiungo wa kati wa nchi ya Hispania Ander Herrera alitolewa nje baada ya kumchezea visivyo mara mbili mshambuliaji Eden Hazard wa timu ya Chelsea.

Taarifa ya FA ilisema kuwa Manchester United inatakiwa kujibu mashtaka hayo hadi kufikia saa kumi na mbili jioni, kwa saa za nchini Uingereza.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment