Afisa mkuu wa jeshi la Sudani kusini amesema wanajeshi watatu wanatuhumiwa kwa makosa ya ubakaji na tayari wamekamatwa. Vikosi vya kijeshi vya waasi na serikali vimekuwa vikishutumiwa kufanya uhalifu wa kivita mara kadhaa nchini humo.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kubi kinachopatikana kilomita 50 kutoka mji mkuu wa Sudani Kusini Juba. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya jeshi nchini humo siku ya Ijumaa, msemai wa jeshi hilo Brigedia Generali Lul Ruai Koang alisema wanajeshi hao wanashikiliwa baada ya taarifa zilizosemekana kwamba takribani wanawake 11 walibakwa ikiwemo msichana wa miaka kumi na mitatu. Mashtaka hayo yamefunguliwa ikiwa ni mwezi sasa tangu rais wa nchi hiyo Salva Kiir kusema kwamba wanajeshi wote ambao walifanya vitendo vya kuwadhalilisha raia ikiwemo kuwabaka wauwawe. Lakini baade alitoa kauli nyingine na kusema watatakiwa wachuliwe hatua za kisheria zinazostahili.
0 comments:
Post a Comment